[{"id":"960","category_id":"8","title":"JAB: TEKNOLOJIA ISITUMIKE KUHARIBU UBORA WA HABARI","photo":"..\/..\/uploads\/gt6a321f1c51bdc7.62536451image_cropper_1781669564473.jpg","news_body":"Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imewataka waandishi wa habari, watangazaji na wadau wa sekta ya habari kutumia teknolojia kwa uwajibikaji ili kuhakikisha maendeleo ya kidijiti hayaathiri ubora wa habari, maadili ya taaluma na haki ya wananchi kupata taarifa sahihi.\n\nKauli hiyo ya Bodi imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula, wakati akijibu swali la Mtangazaji Hassan Dambaya katika kipindi cha Hello Tanzania kinachorushwa na Uhuru FM, aliyetaka kujua Bodi imejiandaaje na kasi ya ukuaji wa teknolojia na matumizi ya Akili Unde inayozidi kuenea kwa kasi ikiwa na athari chanya na hasi?\n\n\u201cTeknolojia inakwenda kasi sana na sisi lazima twende nayo hivyo hivyo kwa sababu ikituacha nyuma na sisi tutakuwa nyuma. Teknolojia hii isipotumika vizuri itakuwa na athari nyingi sana lakini ikitumika vizuri itatusaidia, sasa ni muhimu kuhakikisha haiwi mbadala wa akili zetu,\u201d amesema Wakili Kipangula akijibu swali hilo.\n\nAmesisitiza kuwa matumizi ya teknolojia yanapaswa kwenda sambamba na uzingatiaji wa sheria, maadili na viwango vya uandishi wa habari ili kulinda uaminifu wa vyombo vya habari mbele ya jamii.\n\nAmeeleza kuwa wananchi ndiyo walengwa wakuu wa maudhui yanayozalishwa na vyombo vya habari, hivyo ni muhimu kuhakikisha taarifa wanazopokea zinakuwa sahihi, zilizofanyiwa uhakiki na zinazochangia maendeleo ya taifa badala ya kupotosha au kuzua migawanyiko kwani sasa Akili Unde imekuwa ikitumiwa siyo tu kutengeneza picha zinazoendana na uhalisia bali hata kuweka maneno ambayo jamii isipojua kuyachuja hujikuta ikipotoshwa.\n\nWakili Kipangula amesisitiza kuwa mustakabali wa tasnia ya habari unategemea uwezo wa wadau wake kuoanisha matumizi ya teknolojia na misingi ya taaluma, huku lengo kuu likiwa ni kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata habari zenye ubora, usahihi na manufaa kwa maendeleo ya jamii.","post_time":"2026-06-17 07:13:23.201757","scope":"scope","rcount":"181"},{"id":"959","category_id":"8","title":"TANZANIA YAPIGA HATUA UPATIKANAJI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA WAFIKIA 29.6%","photo":"..\/..\/uploads\/gt6a321ea1976f52.06714622image_cropper_1781669415725.jpg","news_body":"TANZANIA imeonyesha mafanikio makubwa katika kupanua upatikanaji wa nishati safi ya kupikia, ambapo kiwango cha kitaifa cha upatikanaji kimeongezeka kutoka asilimia 6.9 mwaka 2021 hadi asilimia 28.6 mwaka 2025.\n\nOngezeko hili la mara nne zaidi, linadhihirisha athari za jitihada mahsusi za serikali, dhamira ya kisiasa na ushirikiano na wadau wa maendeleo pamoja na sekta binafsi.\n\nKamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo Juni 15, 2026, wakati wa Maadhimisho ya Miaka 13 ya Mpango wa Energising Development (EnDev) nchini.\n\nAmesema mafanikio hayo yanaonyesha dhamira ya Tanzania kuhakikisha wananchi wanapata nishati safi, salama na nafuu ya kupikia.\n\nAmesema kuwa chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kupikia safi kumepewa kipaumbele cha kitaifa na kuingizwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2050.\n\nMhandisi Luoga ameeleza kuwa, Mkakati wa Kitaifa wa Kupikia Safi 2024\u20132034 unalenga kufikia asilimia 80 ya upatikanaji wa kupikia safi ifikapo mwaka 2034, huku National Energy Compact 2025\u20132030 ikilenga asilimia 75 ifikapo mwaka 2030.\n\nAmeongeza kuwa ingawa kumekuwa na mafanikio, zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania bado wanategemea kuni na mkaa, hali inayochangia uchafuzi wa hewa majumbani, uharibifu wa mazingira na mzigo wa muda kwa wanawake na watoto.\n\nKupitia mpango wa EnDev, changamoto hizi zimepunguzwa kwa kusambaza teknolojia nafuu na bora za kupikia, hususan Jiko Matawi linalozalishwa nchini.\n\nMajiko hayo hupunguza matumizi ya kuni kwa hadi asilimia 40, kuboresha ustawi wa kaya na kusaidia uhifadhi wa misitu pamoja na juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.\n\nTangu mwaka 2013 hadi 2026, EnDev imefanikisha upatikanaji wa suluhisho za taa za sola kwa takribani watu 300,000 na suluhisho za kupikia safi kwa watu milioni 2 kupitia majiko bora na teknolojia za kupikia kwa umeme.\n\nMpango huu umewezesha zaidi ya wazalishaji 120 wa Jiko Matawi kufanya kazi katika mikoa 20, na hivyo kuunda ajira na kuimarisha ujasiriamali wa ndani.\n\nAidha, Mhandisi Luoga amesifu kuanzishwa kwa Chama cha Kitaifa cha Wazalishaji wa Jiko Matawi, akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuunda mazingira wezeshi kupitia mageuzi ya sera, uendelezaji wa masoko na upatikanaji wa fedha. Amesema mafanikio ya EnDev yanatoa msingi thabiti wa kupanua suluhisho za nishati safi na kuboresha maisha ya mamilioni ya kaya nchini.\n\nKwa upande wake, Mkurugenzi wa SNV Tanzania, Mary Rauscher, amesema kwa zaidi ya muongo mmoja, EnDev imepanua upatikanaji wa nishati safi, nafuu na endelevu kwa karibu watu milioni 2, hususan vijijini na maeneo yaliyokuwa hayajahudumiwa.\n\nAmeongeza kuwa kupitia mbinu za soko, mpango huu umechochea ukuaji wa sekta binafsi, kuwawezesha wajasiriamali wa ndani na kuimarisha mnyororo mzima wa thamani kuanzia kupikia safi hadi suluhisho za solar off-grid.\n\nRauscher amesisitiza kuwa maendeleo endelevu yanahitaji mageuzi ya mifumo katika sekta za nishati, kilimo na maji.\n\nAmesema SNV inalenga kuimarisha taasisi, kuwezesha masoko jumuishi na kushughulikia mizizi ya ukosefu wa usawa.\n\nAmesisitiza kuwa usawa wa kijinsia na ujumuishaji wa kijamii ni kiini cha kazi zao, kuhakikisha wanawake, vijana na makundi yaliyotengwa si wadau pekee bali pia ni wahamasishaji wakuu wa mabadiliko.","post_time":"2026-06-17 07:11:19.946808","scope":"scope","rcount":"90"},{"id":"958","category_id":"8","title":"REA YAWAALIKA WADAU KUTEMBELEA BANDA WIKI YA UTUMISHI KWA UMMA CHINANGALI","photo":"..\/..\/uploads\/gt6a321df18b24b2.79606533image_cropper_1781669255708.jpg","news_body":"Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Bw. Renatus Msangira kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), leo Juni 16, 2026 amewaongoza watumishi wa REA katika kuwaeleza wadau kuhusiana na miradi mbalimbali inayotekelezwa, hatua iliyofikiwa na mipango iliyopo kwa wannachi wanaotembelea banda la REA katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi kwa Umma 2026 yaliyoanza leo jijini Dodoma.\n\nMaadhimisho ya mwaka huu yamepambwa na kaulimbiu inayosema \u201cKuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu","post_time":"2026-06-17 07:08:23.916705","scope":"scope","rcount":"41"},{"id":"957","category_id":"8","title":"WATUMISHI SABA MANYONI NA MZABUNI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA UTAKATISHAJI FEDHA MILIONI 501","photo":"..\/..\/uploads\/gt6a321d7da02809.65617111image_cropper_1781669159050.jpg","news_body":"Watumishi saba wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni pamoja na mzabuni mmoja wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Manyoni wakikabiliwa na mashtaka mbalimbali ya uhujumu uchumi yakiwemo utakatishaji fedha unaodaiwa kuhusisha zaidi ya Sh milioni 501 za Serikali.\n\nKesi hiyo ya Uhujumu Uchumi Na. 13485\/2026 ilifunguliwa Juni 16, 2026 dhidi ya aliyekuwa Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, George Mzeru, pamoja na maafisa mahesabu Emilian Mauki, Lutufyo Mwakapala, Edward Kilumbu, Revania Ruheta, Doreen Shirima na Salum Mafita. Mshitakiwa mwingine ni mzabuni wa kampuni ya ML Kimboka General Trading, Michael Mushi.\n\nWashtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka sita ambayo ni utakatishaji fedha, kuongoza genge la uhalifu, kuisababishia mamlaka husika hasara, wizi wakiwa watumishi wa umma, ufujaji pamoja na ubadhirifu.\n\nUpande wa mashtaka ulidai kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo kati ya Julai 1, 2024 hadi Mei 29, 2026 na kusababisha hasara kwa Serikali.\n\nMashtaka hayo yalisomwa mahakamani na Wakili wa Serikali, Godfrey Songolo, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Manyoni, Ailisile Mwankejela.\n\nWashtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi wala kutoa dhamana.\n\nKesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 30, 2026 kwa ajili ya kutajwa huku uchunguzi ukiendelea.","post_time":"2026-06-17 07:06:27.798586","scope":"scope","rcount":"77"},{"id":"956","category_id":"8","title":"MAGARI MABOVU 07 YAKAMATWA, MADEREVA WENYE LESENI ZILIZOISHA MUDA WACHUKULIWA HATUA-SONGWE.","photo":"..\/..\/uploads\/gt6a321cccb46ce0.92431767image_cropper_1781668948017.jpg","news_body":"Magari saba (07) yaliyobainika kuwa na ubovu mkubwa yameondolewa namba za usajili, mengine yakatozwa faini huku baadhi yakielekezwa kurekebisha kasoro mbalimbali za kiufundi, kufuatia operesheni maalumu ya ukaguzi wa magari yanayotoa huduma za usafiri wa abiria iliyofanywa na Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Songwe katika Wilaya ya Songwe na vijiji vyake, kwa lengo la kuimarisha usalama wa abiria na watumiaji wengine wa barabara.\n\nAkizungumza Juni 16, 2026 wakati wa operesheni hiyo, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Joseph Bukombe alisema operesheni hiyo, itakayoendelea hadi mwisho wa mwezi Juni, inalenga kuhakikisha magari yote yanayosafirisha abiria yanazingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani ili kulinda maisha ya wananchi na kupunguza ajali zinazoweza kuzuilika.\n\nACP Bukombe alisema ukaguzi uliofanyika umebaini baadhi ya magari kubeba abiria kupita kiwango kilichoruhusiwa, kutumia matairi yaliyochakaa, pamoja na kuwa na hitilafu katika mifumo ya usalama ikiwemo spring na shock absorber, ikiwa baadhi ya madereva walikutwa wakiendesha vyombo vya moto wakiwa na leseni zilizoisha muda wake, jambo ambalo ni kinyume na sheria za usalama barabarani.\n\nKatika hatua nyingine, ACP Bukombe alisema operesheni hiyo imebaini baadhi ya wasafirishaji kutowapatia abiria tiketi za kielektroniki kama inavyotakiwa kisheria na badala yake kutoa tiketi za kawaida, hali inayochangia upotevu wa mapato ya Serikali na kuwanyima abiria haki na stahiki zao.\n\nMwisho, ACP Bukombe amesisitiza kuwa operesheni hiyo itaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha huduma za usafiri vijijini zinatolewa kwa kuzingatia sheria, usalama na maslahi ya wananchi.","post_time":"2026-06-17 07:03:31.205126","scope":"scope","rcount":"61"},{"id":"955","category_id":"8","title":"JESHI LA MAGEREZA LASHIRIKI MAADHIMISHO YA KITAIFA YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026","photo":"..\/..\/uploads\/gt6a321c31897a75.84768020image_cropper_1781668812441.jpg","news_body":"Jeshi la Magereza kwa mara nyingine tena linashiriki kikamilifu kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2026 Maadhimisho ambayo ni moja ya Maazimio ya Umoja wa Afrika (AU). \n\nHivyo, Jeshi la Magereza linawakaribisha wananchi wote wa Tanzania kutembelea Banda la Magereza katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma kuanzia Leo Juni 16 hadi 23, 2026.\n\nMaonesho hayo yatawakutanisha Wananchi, Taasisi za Umma na Wadau mbalimbali kwa lengo la kuelezea Dhima, Dira, Mafanikio, Changamoto zilizopo katika suala zima la urekebishaji Wafungwa, kutoa huduma na taarifa mbalimbali muhimu kuhusu shughuli zinazotolewa na Serikali kwa Wananchi kupitia Jeshi la Magereza na kuueleza Umma juu ya Mageuzi ya kisayansi yanayofanywa sasa na Jeshi katika uendeshaji na urekebishaji Wafungwa.\n\nPamoja na kutoa huduma hizo, Jeshi la Magereza kupitia Maadhimisho haya linatoa elimu kwa umma kuhusu huduma zinazotolewa kwa wafungwa na mahabusu pamoja na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali zinazofanywa Magerezani kama mbinu za urekebishaji wafungwa. Wananchi pia wanapata fursa ya kuuliza maswali, kutoa maoni na kupata ufafanuzi wa papo kwa papo kutoka kwa Maafisa Magereza waliopo katika Banda hilo.\n\nSambamba na utoaji wa huduma hizo, Jeshi la Magereza linaendelea kutoa elimu kuhusu shughuli za urekebishaji wa wafungwa, ikiwemo elimu ya maadili, stadi za maisha, mafunzo ya ufundi stadi, ushauri nasaha na programu nyingine zinazolenga kuwawezesha wafungwa kubadilika na kujiandaa kurejea katika jamii wakiwa raia wema na wenye tija kwa familia zao na Taifa kwa ujumla.\n\nKupitia elimu hiyo, wananchi wanahamasishwa kutambua mchango wa Programu za urekebishaji katika kupunguza uhalifu nchini, kuwajengea wafungwa uwezo wa kujitegemea na kuimarisha usalama wa jamii kwa ujumla.\n\nAidha, elimu hiyo inalenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kushirikiana na Jeshi la Magereza katika mchakato wa urekebishaji na urejeshwaji wa wafungwa katika jamii baada ya kutumikia vifungo vyao na kuondoa unyanyapaa hivyo kuwapokea na kuwashirikisha Wafungwa wanaorudi kutoka Magerezani katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.\n\nMaadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi kwa Umma 2026 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo: \u201cKuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu.\u201d","post_time":"2026-06-17 07:00:56.124502","scope":"scope","rcount":"33"},{"id":"954","category_id":"10","title":"UFARANSA YAANZA KOMBE LA DUNIA KWA USHINDI DHIDI YA SENEGAL","photo":"..\/..\/uploads\/gt6a321bbf3fa655.52536749image_cropper_1781668703913.jpg","news_body":"Timu ya Taifa ya Ufaransa imeanza vyema kampeni yake ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Senegal katika mchezo wa Kundi I uliochezwa Juni 16, 2026 nchini Marekani. \n\nBaada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya bila kufungana, Ufaransa iliongeza kasi kipindi cha pili na kufungua ukurasa wa mabao kupitia nahodha wake, Kylian Mbapp\u00e9, aliyefunga dakika ya 66. Mshambuliaji huyo alirejea tena wavuni dakika za nyongeza na kufunga bao lake la pili huku Bradley Barcola akiongeza bao lingine, na kuifanya Ufaransa kuondoka na pointi tatu muhimu. ","post_time":"2026-06-17 06:59:01.319521","scope":"scope","rcount":"116"},{"id":"953","category_id":"8","title":"HABARI PICHA: KAIMU KAMISHNA WA USTAWI WA JAMII AKUTANA NA WATOTO KATIKA KONGAMANO LA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KIKOMBO","photo":"..\/..\/uploads\/gt6a321b257c4bb0.22853969image_cropper_1781668551437.jpg","news_body":"Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Faithmary Lukindo akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo katika Kongamano la Maadimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika lililofanyika leo Juni 16, 2026 katika Makao ya Taifa Watoto Kikombo.\n\nKongamano hilo la siku moja, limewakutanisha watoto kutoka katika Kata za Kikombo, Ihumwa na Mtumba likiwa na kaulimbiu inayosema \u201cMtoto ni Malezi Msingi wa Familia Bora kwa Taifa Imara.\u201d Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika ufanyika kila tarehe 16 Juni kila mwaka .","post_time":"2026-06-17 06:56:28.091624","scope":"scope","rcount":"26"},{"id":"952","category_id":"10","title":"UBELGIJI NA MISRI WAGAWANA POINTI BAADA YA SARE YA 1\u20131","photo":"..\/..\/uploads\/gt6a30de59048db0.43777035image_cropper_1781587465837.jpg","news_body":"Belgium imetoka sare ya 1\u20131 na Egypt katika mchezo wa Kombe la Dunia 2026. , uliochezwa Juni 15,2026\n\nEgypt walipata goli la kwanza kupitia Emam Ashour dakika ya 20. Belgium wakasawazisha kupitia Goli la Kujifunga Kwa Beki wa Misri kipindi cha pili.","post_time":"2026-06-16 08:24:47.831476","scope":"scope","rcount":"16"},{"id":"951","category_id":"10","title":"JUST AFUNGA MAWILI, IRAN YACHOMOA SARE YA 2-2","photo":"..\/..\/uploads\/gt6a30dd0c5dd932.94510102image_cropper_1781587132072.jpg","news_body":"Iran na New Zealand zimetoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa Kundi G wa Kombe la Dunia, huku mshambuliaji wa Motherwell, Just, akifunga mabao mawili kwa upande wa New Zealand.\n\nIran ilifanikiwa kusawazisha kupitia bao la ustadi la Rezaeian, aliyefunga kwa mpira wa kisigino na kurejesha matumaini ya timu yake.\n\nBaadaye, Mohebbi aliifungia Iran bao la pili la kusawazisha baada ya New Zealand kuongoza tena, na kuhakikisha timu hizo zinagawana pointi.\n\nMatokeo hayo yanafuatia sare nyingine ya mabao 1-1 katika kundi hilo kati ya Ubelgiji na Misri, hali inayofanya ushindani wa Kundi G kuwa mkali zaidi.","post_time":"2026-06-16 08:19:15.155471","scope":"scope","rcount":"16"},{"id":"950","category_id":"8","title":"MCHENGERWA AWEKA AJENDA YA MAGEUZI KWA BODI YA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA Mt. MERU, ATAKA UONGOZI WA MATOKEO","photo":"..\/..\/uploads\/gt6a2a6189402d06.92821535image_cropper_1781162265040.jpg","news_body":"Waziri wa Afya, Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa, ameitaka Bodi mpya ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mt. Meru kuongoza kwa mtazamo wa mageuzi na kusukuma mbele mabadiliko yenye tija yatakayoboresha utoaji wa huduma za afya na matokeo ya afya kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.\n\nAkizungumza katika hafla rasmi ya uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya hospitali hiyo iliyofanyika leo katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha, Mheshimiwa Mchengerwa alisema sekta ya afya nchini inaingia katika hatua mpya ambapo mafanikio ya viongozi yatapimwa kwa matokeo halisi na mchango wao katika kuboresha maisha ya wananchi badala ya taratibu za kiutawala pekee.\n\n\u201cLeo si uzinduzi wa Bodi pekee. Ni uzinduzi wa matarajio mapya, kiwango kipya cha uongozi na sura mpya ya utoaji wa huduma za afya katika Arusha na Tanzania kwa ujumla,\u201d alisema Mheshimiwa Mchengerwa.\n\nWaziri Mchengerwa aliwapongeza Mwenyekiti na Wajumbe wapya wa Bodi kwa kuteuliwa kushika nafasi\n\nhizo muhimu, akisisitiza kuwa uteuzi wao unaambatana na wajibu mkubwa wa kusimamia moja ya hospitali\n\nmuhimu za rufaa nchini inayohudumia maelfu ya Watanzania wanaohitaji huduma bora, salama na za wakati.\n\nKusukuma Mageuzi ya Sekta ya Afya\n\nMheshimiwa Mchengerwa alisisitiza dhamira ya Serikali ya kuharakisha mageuzi katika sekta ya afya na\n\nkuitaka Bodi hiyo kwenda zaidi ya majukumu ya kawaida ya usimamizi na kuwa chachu ya ubunifu,\n\nuwajibikaji na ubora wa taasisi.\n\n\u201cSikuja Wizara ya Afya kusimamia mifumo iliyopo. Nimekuja kuharakisha mabadiliko,\u201d alisema.\n\nAlieleza kuwa taasisi za afya zinapaswa kuongozwa kwa kuzingatia matokeo, kutumia takwimu katika\n\nkufanya maamuzi, kuweka mgonjwa katikati ya huduma, na kuwajibika katika kuhakikisha uwekezaji wa\n\nfedha za umma unaleta manufaa kwa wananchi.\n\nWaziri Mchengerwa aliitaka Bodi kufuatilia kwa karibu utendaji wa hospitali, kuuliza maswali muhimu na\n\nkuhakikisha uongozi wa hospitali unaendelea kuzingatia maboresho yanayopimika katika utoaji wa huduma.\n\nMsisitizo wa Matokeo Yanayopimika\n\nMojawapo ya ujumbe muhimu katika hotuba ya Waziri ulikuwa ni umuhimu wa usimamizi unaozingatia\n\nmatokeo.\n\nAliwahimiza wajumbe wa Bodi kuzingatia viashiria vya utendaji kama vile kupungua kwa vifo vya akina\n\nmama wajawazito, kuongezeka kwa kuridhika kwa wagonjwa, kupungua kwa muda wa kusubiri huduma,\n\nkuongezeka kwa mapato ya ndani ya hospitali, na kuboreshwa kwa ubora wa huduma.\n\n\u201cHatupaswi kupima mafanikio kwa kiasi cha fedha kilichotumika. Tunapaswa kupima mafanikio kwa maisha\n\nyaliyookolewa,\u201d alisema Mheshimiwa Mchengerwa.\n\nAidha, alisisitiza matumizi ya takwimu na ushahidi katika kufanya maamuzi na kuendesha maboresho\n\nendelevu katika shughuli zote za hospitali.\n\nKuweka Mgonjwa Katikati ya Huduma\n\nWaziri Mchengerwa alithibitisha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha wagonjwa wanabaki kuwa kitovu cha\n\nutoaji wa huduma za afya.\n\nAlieleza kuwa uwepo wa majengo bora na vifaa vya kisasa pekee hauwezi kuifanya hospitali kuwa yenye\n\nmafanikio ikiwa wagonjwa hawapati huduma zenye utu, huruma na taaluma.\n\n\u201cKipimo halisi cha mafanikio ya hospitali si ukubwa wa majengo yake. Ni kiwango cha imani ambacho\n\nwananchi wanakiweka katika hospitali hiyo,\u201d alisema.\n\nMheshimiwa Mchengerwa alitoa wito wa kuboresha huduma kwa wagonjwa katika maeneo yote ya utoaji\n\nhuduma ikiwemo mapokezi, maabara, maduka ya dawa, wodi na vitengo vya huduma za dharura.\n\nKukumbatia Ubunifu wa Kidijitali\n\nAkizungumzia nafasi ya teknolojia katika mageuzi ya sekta ya afya, Waziri aliitaka Hospitali ya Rufaa ya\n\nMkoa Mt. Meru kuwa kinara wa ubunifu wa kidijitali katika huduma za afya.\nAlitaja matumizi ya kumbukumbu za afya za kidijitali, huduma za tiba kwa njia ya mtandao (telemedicine),\nna mifumo ya kidijitali ya usimamizi wa dawa, fedha, vifaa tiba na huduma kwa wagonjwa kuwa miongoni\nmwa maeneo muhimu ya kupewa kipaumbele.\n\u201cHospitali ya karne ya 21 haiwezi kuendeshwa kwa mifumo ya karne iliyopita,\u201d alisema.\nKuimarisha Ushirikiano wa Kimkakati\nAkigusia umuhimu wa Mkoa wa Arusha kama kitovu cha biashara, utalii, diplomasia na uwekezaji,\nMheshimiwa Mchengerwa aliihimiza Bodi kujenga ushirikiano na sekta binafsi, taasisi za elimu ya juu,\nwashirika wa maendeleo na taasisi za utafiti.\nAlisema ushirikiano wa kimkakati unaweza kufungua fursa za rasilimali zaidi, utaalamu na teknolojia\nzitakazosaidia kuimarisha huduma za afya na kunufaisha jamii.\nDhamira ya Kuboresha Matokeo ya Afya\nKatika hitimisho la hotuba yake, Waziri Mchengerwa aliwakumbusha wajumbe wa Bodi kuwa maamuzi yao\nyana athari za moja kwa moja kwa wagonjwa na familia zinazotegemea hospitali hiyo kupata huduma.\n\u201cKila uamuzi mnaoufanya unaweza kuokoa maisha. Kila ubunifu mnaouanzisha unaweza kuboresha huduma.\nKila mfumo mnaouimarisha unaweza kurejesha matumaini ya wananchi,\u201d alisema.\nMheshimiwa Mchengerwa alieleza imani yake kuwa chini ya uongozi wa Bodi mpya, Hospitali ya Rufaa ya\nMkoa Mt. Meru itaendelea kuwa mfano wa kitaifa wa ubora, ubunifu, uwajibikaji na mageuzi ya sekta ya afya\nkwa kuendana na Ajenda ya Mageuzi ya Afya Tanzania 2023\u20132030.\nWaziri Mchengerwa alitangaza rasmi uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mt. Meru,\nhatua inayofungua ukurasa mpya wa uongozi na mageuzi kwa moja ya taasisi muhimu zaidi za afya Kaskazini mwa Tanzania.","post_time":"2026-06-11 10:19:33.961447","scope":"scope","rcount":"72"},{"id":"949","category_id":"8","title":"MKUU WA JESHI LA MAGEREZA AFUNGUA MAFUNZO YA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA UREKEBISHAJI KWA MAAFISA USTAWI WA JAMII","photo":"..\/..\/uploads\/gt6a2a60aee18c00.01114184image_cropper_1781162099268.jpg","news_body":"Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, leo Juni 10, 2026, amefungua rasmi Mafunzo kwa Maafisa Ustawi wa Jamii kuhusu Mwongozo wa Utekelezaji wa Programu za Urekebishaji katika Ukumbi wa Rugimbana, Msalato, jijini Dodoma.\n\nAkizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, CGP Katungu aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kwa namna inavyoendelea kuliwezesha Jeshi la Magereza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Alisema Serikali imekuwa ikitoa rasilimali fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya magereza, makazi ya watumishi, vyombo vya usafiri pamoja na kugharamia mafunzo mbalimbali kwa watumishi wa Jeshi la Magereza.\n\nCGP Katungu alibainisha kuwa moja ya majukumu ya msingi ya Jeshi la Magereza ni urekebishaji wa wafungwa kwa kuwapatia elimu, ujuzi na maarifa ili wanapomaliza vifungo vyao warejee katika jamii wakiwa raia wema na wenye tija. Alieleza kuwa jukumu hilo limeainishwa katika Sheria ya Magereza, Sura ya 58, Kanuni Na. 62 pamoja na Kanuni za Kudumu za Magereza (Prisons Standing Orders, 2003, 4th Edition), Kanuni Na. 404. Aidha, sheria za kimataifa pamoja na mikataba na matamko mbalimbali ya kikanda vimeendelea kusisitiza umuhimu wa urekebishaji wa wafungwa kwa lengo la kuwajengea ujuzi na maarifa yatakayowasaidia baada ya kumaliza vifungo vyao.\n\nAliongeza kuwa Mheshimiwa Rais amekuwa akielekeza Jeshi la Magereza kuimarisha utekelezaji wa majukumu yake, hususan katika eneo la urekebishaji wa wafungwa ili waweze kurejea katika jamii wakiwa na mchango chanya wa maendeleo. Vilevile, Tume ya Kuboresha Mfumo wa Haki Jinai ilitoa mapendekezo mbalimbali yanayolihusu Jeshi la Magereza, ikiwemo kuboresha programu za urekebishaji wa wafungwa. Sambamba na hilo, Ukaguzi wa Ufanisi (Performance Audit) uliofanywa mwaka 2024 na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (CAG) ulipendekeza kuandaliwa na kutekelezwa kwa Mwongozo wa Utekelezaji wa Programu za Urekebishaji.\n\nKutokana na maelekezo na mapendekezo hayo, Jeshi la Magereza limeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha utekelezaji wa jukumu la urekebishaji. Miongoni mwa hatua hizo ni kuandaa mitaala mipya ya mafunzo kwa watumishi pamoja na kuimarisha ushirikiano na taasisi mbalimbali za Serikali, ikiwemo Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) katika utoaji wa mafunzo kwa wafungwa na watumishi.\n\nKatika hatua nyingine, Jeshi la Magereza limeandaa Mwongozo wa Utekelezaji wa Programu za Urekebishaji wa Wafungwa unaobainisha hatua kuu nne za mzunguko wa urekebishaji (Rehabilitation Circle). Hatua hizo ni mapokezi na maelekezo ya awali gerezani (Admission and Orientation), kipindi cha kutumikia kifungo na kupatiwa huduma za urekebishaji (Incarceration Period), maandalizi ya kuachiliwa (Pre-Release) na hatua ya kurejea na kuunganishwa tena katika jamii (Reintegration).\n\nAlisema mwongozo huo utamwezesha kila mfungwa kufanyiwa tathmini ya kina ili kubaini mahitaji yake na kuingizwa katika programu stahiki za urekebishaji. Hadi sasa, makundi yaliyokwisha kupatiwa mafunzo hayo ni Maafisa Mapokezi, Wakuu wa Magereza yote nchini, na sasa wataalamu wa Ustawi wa Jamii, Saikolojia na Sosholojia.\n\nAidha, CGP Katungu alisema Jeshi la Magereza limeanza kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwa vitendo, ambapo utafiti kuhusu urudiaji wa makosa kwa wafungwa waliomaliza vifungo vyao umeanza kufanyika kwa ushirikiano na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashariki kilichopo Dar es Salaam. Kwa sasa, wataalamu hao wanaendelea na ukusanyaji wa takwimu kwa ajili ya utafiti huo.\n\nPia, Jeshi la Magereza limeunda timu maalumu ya kuandaa andiko la kuanzisha Mfuko Maalumu wa Kuwasaidia Wafungwa Wanaomaliza Vifungo vyao ili kuwawezesha kujitegemea wanaporejea katika jamii. Vilevile, Jeshi linaendelea kuunda Mfumo wa Kuhifadhi Taarifa za Wafungwa (PIPMIS) kwa kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao (e-GA), ambapo utekelezaji wake umefikia hatua nzuri.\n\nAkiwasilisha taarifa ya mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Sehemu ya Huduma za Usimamizi wa Wafungwa ya Jeshi la Magereza, SACP Emmanuel Malisa, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Edith Mbogo, alisema mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha Maafisa Ustawi wa Jamii kuelewa na kutekeleza ipasavyo Mwongozo wa Urekebishaji wa Mwaka 2025. Alibainisha kuwa mafunzo hayo ni mwendelezo wa awamu zilizopita na yanakusudia kuimarisha usimamizi wa programu za urekebishaji, kuwajengea washiriki uwezo wa kitaaluma na kuchangia urejeshwaji bora wa wafungwa katika jamii.","post_time":"2026-06-11 10:15:55.772290","scope":"scope","rcount":"65"},{"id":"948","category_id":"8","title":"MANISPAA YA KIBAHA YATOA SH MILIONI 991 KWA VIKUNDI 51","photo":"..\/..\/uploads\/gt6a2a6020d4a1a5.13903174image_cropper_1781161971640.jpg","news_body":"Vikundi 51 vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu katika Manispaa ya Kibaha, mkoani Pwani, vimenufaika na mikopo yenye thamani ya Sh milioni 991.54 kupitia asilimia 10 ya mapato kwa mwaka wa fedha 2025\/2026.\n\nVikundi hivyo vinaweka jumla ya vikundi 2,273 ambavyo tayari vimenufaika na mikopo hiyo katika Manispaa hiyo kwa kipindi hicho.\n\nAkizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo kwa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025\/2026, Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Silvestry Koka, aliielekeza Manispaa ya Kibaha kuhakikisha wajasiriamali wanaopata mikopo hiyo wanapatiwa mafunzo yatakayowasaidia kukuza na kuendeleza biashara zao.\n\n\u201cHakuna biashara ndogo, Msikatishwe tamaa na maneno ya watu, Fanyeni kazi kwa bidii, muwe wabunifu na muendelee kupanua biashara zenu ili siku moja muwe wafanyabiashara wakubwa,\u201d aliwasihi Koka.\n\nPia alimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rafiki ya upatikanaji wa mitaji kwa wananchi kupitia mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani, hatua ambayo imepunguza utegemezi wa mikopo yenye riba kubwa kutoka taasisi za kifedha.\n\n\u201cLeo tunashuhudia jinsi mpango huu unavyoendelea kuleta tija kwa makundi maalum na kuinua maisha yao kiuchumi,\u201d aliongeza Koka.\n\nMkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha, Dkt. Rogers Shemwelekwa, alieleza kati ya Sh milioni 991.54 zilizotolewa, Sh milioni 359 zimetengwa kwa vikundi 17 vya wanawake, Sh milioni 557.04 kwa vikundi 25 vya vijana na Sh milioni 75.5 kwa vikundi vya watu wenye ulemavu.\n\nDkt. Shemwelekwa alifafanua kuwa miradi iliyokopeshwa kwa vikundi hivyo ni usafirishaji, ambapo pikipiki 25, gari moja aina ya Toyota na bajaji nne zimenunuliwa, ufugaji wa kuku, uchomeleaji, ushonaji, utengenezaji wa batiki, sabuni na kilimo cha umwagiliaji.\n\nKwa upande wake, mnufaika wa mikopo hiyo kutoka kundi la watu wenye ulemavu, Amos Mhongole, alibainisha awali kikundi chao kilipatiwa Sh milioni 46 na kutokana na urejeshaji mzuri wa mkopo huo, wameongezewa mtaji.\n\nKadhalika aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuweka mazingira yanayowainua wajasiriamali wadogo na kuwawezesha kupanua shughuli zao za kiuchumi.\n\nKwa mujibu wa Manispaa ya Kibaha, bajeti ya asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa makundi maalum katika mwaka wa fedha 2025\/2026 ni Sh bilioni 1.099, fedha za marejesho ya mikopo zinatarajiwa kufikia zaidi ya Sh bilioni 1.9, huku bakaa ya miaka ya fedha 2022\/2023 na 2023\/2024 ikiwa Sh bilioni 1.1 na Sh milioni 632.9 , na kufanya jumla ya fedha kwa utoaji wa mikopo kufikia Sh bilioni 4.805.","post_time":"2026-06-11 10:13:32.964219","scope":"scope","rcount":"28"},{"id":"947","category_id":"8","title":"RAIS DKT. MWINYI AFANYA MAZUNGUMZO NA MGENI WAKE RAIS WA SINGAPORE IKULU ZANZIBAR","photo":"..\/..\/uploads\/gt6a2a5f7ea879a7.48472219image_cropper_1781161807011.jpg","news_body":"Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 10 Juni 2026, Ikulu Zanzibar, amempokea mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Tharman Shanmugaratnam, na kufanya naye mazungumzo Ikulu Zanzibar pamoja na ujumbe wake.\n\nRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amempokea Rais wa Jamhuri ya Singapore Mhe.Tharman Shanmugaratnam,katika Ikulu ya Zanzibar, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi nchini Tanzania iliyoanza Juni 8, 2026.\n\nKikao hicho cha ngazi ya juu kimejikita katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kupanua ushirikiano wa kiuchumi kati ya Zanzibar na Singapore, hususan katika sekta zenye tija kwa maendeleo ya pande zote mbili.\n\nMazungumzo hayo yameangazia maeneo muhimu ya kimkakati ikiwemo utalii wa kiwango cha juu (high-value tourism), uwekezaji, maendeleo ya rasilimali watu, pamoja na ushirikiano katika sekta ya usafirishaji na mifumo ya ugavi (logistics), ambayo imeelezwa kuwa msingi muhimu wa ukuaji wa uchumi wa kisasa.\n\nViongozi hao pia wamejadili namna ya kuimarisha Mpango wa Ushirikiano wa Singapore (Singapore Cooperation Programme), ambao umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa katika mafunzo na kujenga uwezo wa wataalamu, hususan katika sekta za maendeleo na utawala bora.\n\nAidha, wamekubaliana kuendeleza sekta ya usindikaji wa mazao na bidhaa ili kuongeza thamani ya rasilimali zilizopo, kukuza ajira na kuimarisha ushindani wa bidhaa katika masoko ya kikanda na kimataifa.\n\nRais Dkt. Mwinyi amesisitiza dhamira ya Zanzibar kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuvutia washirika wa kimataifa, akibainisha kuwa ushirikiano na Singapore ni fursa muhimu ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi, kijamii pamoja na uzalishaji wa nishati hasa wa gesi asilia\n\nKwa upande wake, Rais wa Singapore Mhe.Tharman amepongeza juhudi za Zanzibar katika kuimarisha uchumi na ameeleza utayari wa nchi yake kuendelea kushirikiana katika sekta za utalii, teknolojia, mafunzo na uwekezaji wa kimkakati.\n\nZiara hiyo inaendelea kuimarisha mahusiano ya kirafiki na kiuchumi kati ya Zanzibar na Singapore, huku pande zote mbili zikieleza matumaini ya kuona ushirikiano huo ukizaa matunda zaidi kwa manufaa ya wananchi wao.","post_time":"2026-06-11 10:10:51.509419","scope":"scope","rcount":"33"},{"id":"946","category_id":"8","title":"SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI \u2013 DKT. MWIGULU","photo":"..\/..\/uploads\/gt6a2a5ef2d5b741.03925052image_cropper_1781161664852.jpg","news_body":"WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kuondoa vikwazo na kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi ili kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.\n\nAmeyasema hayo leo (Jumatano, Juni 10, 2026), wakati akizindua ghala la forodha la kampuni ya Ciwaye Trading Co. Ltd Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.\n\n\u201cKama tunavyoheshimu sekta ya umma, tunatakiwa kuheshimu sekta binafsi kwa uzito ule ule, kama mataifa mengine yaliyoendelea, uchumi wa mataifa hayo nguzo yake ni sekta binafsi.\u201d\n\nDkt. Mwigulu aliongeza kwa kusema \u201cKwa kuheshimu hilo, nimeona nije kuzindua mradi huu, kama ambavyo nimepita kwenye ziara kuzindua miradi ya Serikali, ndiyo maana nimeona na hapa nije mwenyewe.\u201d\n\nAidha, ameeleza kuwa mradi huo una umuhimu mkubwa katika maendeleo ya nchi, hivyo hauna budi kulelewa.\n\n\u201cUkubwa wa jambo hili haupimwi kwa majengo, bali kwa uthubutu na matokeo yanayoakisi Dira yetu ya maendeleo na maono ya Rais wetu ya kuhakikisha mradi kama huu unatoa matokeo yaliyokusudiwa.\u201d Amesisitiza Waziri Mkuu Mwigulu.\n\nWaziri Mkuu ameongeza kuwa mradi huo unatazamwa na Serikali kama mradi wa kielelezo wa kutekeleza Dira 2050 na ndiyo maana Serikali imekuwa ikiboresha mazingira ya uwekezaji nchini, ikiwemo maboresho ya sheria za uwekezaji.\n\n\u201cZimebadilishwa Sheria za uwekezaji ili kuhakikisha wazawa wananufaika na kuushika uchumi, zamani vivutio vya uwekezaji viliwanufaisha wageni, lakini sasa wazawa wanapata vivutio hivyo,\u201d ameeleza Waziri Mkuu.\n\nAmeongeza kuwa: \u201cMfano katika sekta ya uzalishaji, zamani miradi yote mikubwa ilikuwa inatekelezwa na wageni, lakini mabadiliko hayo ya sheria yamewezesha wazawa kutekeleza miradi mikubwa, na sasa wanaweza kuajiri wageni katika utekelezaji wa miradi hiyo.\u201d\n\nWaziri Mkuu Mwigulu amesema mkakati mwingine unaoenda sambamba na mabadiliko ya sheria, ni pamoja na kuondoa zaidi ya tozo 270 ili kuwapunguzia mzigo wafanyabiashara na walaji wa mwisho.\n\nAkizungumzia utekelezaji wa mradi huo, Waziri Mkuu ameeleza kufurahishwa na hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wake, kwani umetekelezwa ndani ya muda mfupi lakini viwango vya ubora vimezingatiwa.\n\nAmesema uamuzi wa kuanzisha ghala hilo mkoani Dodoma ni wa kimkakati kwani Dodoma ipo katikati ya nchi, ikiunganisha maeneo mengine ya nchi na fursa zilizopo katika maeneo hayo, ambapo amewataka wafanyakazi wa mradi huo kuwa waaminifu ili mradi uwe na faida endelevu, kwao binafsi na jamii.\n\nPia Waziri Mkuu Mwigulu amewahimiza Wakuu wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhamasisha wawekezaji kuwekeza kwenye mikoa na maeneo yao kwa kuweka miundombinu inayochochea vyanzo vya mapato na kukua kwa uchumi.\n\nKatika hatua nyingine, Waziri Mkuu Mwigulu ameuagiza Wakala wa Barabara za Mijini na Vijini (TARURA) kukaa kwa haraka na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na kufanya tathmini ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami ya kilometa 25 kuanzia Chamwino kwenda kituo cha treni cha Igandu ili kusaidia ufanisi wa ghala lililojengwa kwani barabara hiyo itaunufaisha mradi huo.\n\nKwa upande wake Meneja Masoko wa ghala hilo, Leroy Nelson amesema mradi huo umegharimu zaidi ya shilingi bilioni tatu ambapo utekelezaji wake umekamilika kwa asilimia 100.","post_time":"2026-06-11 10:08:31.668577","scope":"scope","rcount":"48"}]